{"id":19542,"date":"2026-09-25T17:38:25","date_gmt":"2026-09-25T16:38:25","guid":{"rendered":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/?p=19542"},"modified":"2026-09-25T17:38:25","modified_gmt":"2026-09-25T16:38:25","slug":"mungu-amebadilisha-maisha-yangu-ya-kiroho","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/blog\/2026\/09\/25\/mungu-amebadilisha-maisha-yangu-ya-kiroho\/","title":{"rendered":"MUNGU AMEBADILISHA MAISHA YANGU YA KIROHO!"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cWatu wa Mungu niungeni katika kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake maishani mwangu. Jina langu ni Fred kutoka Ghana. Ushuhuda wangu ni huu: Nilianza kujiunga na maombi shirikishi ya Ndugu Chris katika God\u2019s Heart TV mwaka wa 2024, naye Mungu akaanza kuyabadilisha Maisha yangu ya kiroho. Nilikuwa na wasiwasi na jakamoyo haswa kuhusu hali yangu ya umaskini na ugumu maishani, ambayo hapo awali ilinifanya nitafute jawabu nje ya mapenzi ya Mungu. Lakini kwa sasa moyo wangu umetulia. Sina wasiwasi wala jakamoyo hata hali iwe ngumu ama yenye uhitaji mkuu. Hali yangu inanilazimisha niutafute uso wa Mungu ili niwe na uhusiano mkuu Naye, na hili limesababisha niwe katika kiwango kipya Naye. Mungu alitenda muujiza mkuu jumamosi ya tarehe 17, Januari 2025. Nilikuwa nahitaji kwa dharura fedha za kumsajili binti yangu katika shule ya wauguzi. Kiwango kilichokuwa kinahitajika ni GH\u20b5 4,000.00. Sikuwa na mahali popote ningepata pesa hizo; kila njia zilikuwa zimefungwa. Nilienda katika maombi ya moja kwa moja ya Ndugu Chris katika Youtube na nikaomba kwa muda wa saa moja, kutoka saa nane hadi saa tisa jioni. Nilimwamini Mungu licha ya kutojua ni vipi ama wapi fedha hizo zitatoka. Watu wa Mungu, kwa kweli Mungu ni msaada wetu katika kila changamoto zetu. Ndugu yangu kutoka nchini Marekani alinitumia kiwango cha GH\u20b5 4,208.00 \u2013 Zaidi ya hitaji langu \u2013 saa tatu jioni hiyo. Namshukuru Mungu kwa msaada wake!<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>\u201cWatu wa Mungu niungeni katika kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake maishani mwangu. Jina langu ni Fred kutoka Ghana. Ushuhuda wangu ni huu: Nilianza kujiunga na maombi shirikishi ya Ndugu Chris katika God\u2019s Heart TV mwaka wa 2024, naye Mungu akaanza kuyabadilisha Maisha yangu ya kiroho. Nilikuwa na wasiwasi na jakamoyo [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":19543,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"content-type":"","footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-19542","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-testimonies"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/19542","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=19542"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/19542\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":19544,"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/19542\/revisions\/19544"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media\/19543"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=19542"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=19542"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/godsheart.tv\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=19542"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}