Maombi ya Kila Siku
“Kile ambacho moyo wako umekishikilia kinaweza kukukamata kwa urahisi. Tunaposhikilia Neno la Mungu mioyoni mwetu, hugeuka kuwa ngome yetu.”
Katika mzunguko wa shughuli za kila siku, tunapataje wasaa wa kutunza maisha yetu ya kiroho? Pamoja na nguvu nyingi kinzani zinazopigania usikivu wetu, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kutumia muda bora kila siku katika Neno Hai la Mungu – chanzo kimoja cha ukweli na uthabiti tunachoweza kukitegemea kila wakati! Kama vile Mathayo 24:35 inavyosema, “Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” Unaposoma machapisho haya yenye mwongozo juu ya kujitoa kwa Mungu kutoka kwa Timu ya God’s Heart TV, tunaomba kwamba Mungu afungue moyo wako kwa hekima Yake na kukusaidia kuona maisha kwa udhahiri – kupitia macho Yake.
MZINGATIE MWALIMU ILI UJIFUNZE SOMO
Yona 4:9-11, “Mungu akamwambia Yona, ‘Je, ni sawa kukasirika kwa ajili ya mmea?’ Naye akasema, ‘Ni sawa kukasirika hata kufa!’ Lakini Bwana akasema, ‘Umeuhurumia mmea ambao hukuufanyia kitu chochote , wala kuuotesha, uliomea usiku mmoja na kuangamia usiku mmoja. Nami sipaswi kuihurumia Ninawi, mji ule mkubwa, ambao ndani yake mna watu zaidi ya mia moja na ishirini elfu, wasioweza kupambanua kati ya mkono wao wa kulia na wa kushoto—na mifugo mingi?’” Somo ambalo Mungu anataka kukufundisha kupitia hali yako ni…
ADUI MKUU WA UKUAJI
Mithali 16:18, "Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia anguko."Watu wa Mungu, hakuna kiwango ambacho Mungu hatafikia linapokuja suala la kukusaidia kukua kiroho. Uvumilivu wake wa kutuona tukibadilika ni mkubwa kuliko ukaidi wetu wa kubadilika. Tukishindwa kujifunza somo, Mungu ataruhusu au kupanga hali nyingine kutufundisha. Swali ni: je, uko tayari kujifunza? Au muhimu zaidi, je, u mnyenyekevu kujifunza? Kwa sababu adui mkubwa wa ukuaji ni kiburi chetu. Mfano wa kiburi ni kuja mbele za Mungu na swali lakini hatuko…
MASOMO YA MUNGU NDIYO BARAKA KUBWA ZAIDI
Ayubu 23:10-11, “Lakini yeye anaijua njia niiendeayo; Atakaponijaribu nitatoka kama dhahabu, Mguu wangu umezishika sana hatua zake; Nimeishika njia yake wala sikukengeuka. Watu wa Mungu, kamwe msisahau ukweli huu wa msingi - changamoto si sehemu tu ya maisha, ni njia ya ukuaji. Kwa hiyo swali si kwamba, ‘Kwa nini ninakabiliwa na changamoto?’ bali, ‘Mungu ananifundisha nini kupitia yale ninayopitia?’ Hii si kwa sababu Mungu hana haki bali ni kwa sababu Yeye ni Baba mwenye upendo ambaye “Humkanya yeye ampendaye, naye…
NJIA BORA YA KUSIMAMIA HAZINA
Mathayo 6:20-21, “Bali jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba. Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.” Enyi watu wa Mungu, kama wageni na wasafiri duniani, tunapotumia vitu vya ulimwengu huu, hatupaswi kujihusisha navyo. Wengi hufuatilia na kujiwekea hazina duniani - vitu wanavyotaka lakini hawavihitaji sana, vitu vinavyopungua thamani pale nondo na kutu vinapoharibu. Katika Luka 12:16-21, Yesu alitoa onyo kali kuhusu hatari za kujiwekea hazina bila kuwa tajiri kwa Mungu…
USIYASONGE MATUNDA YA NENO LA MUNGU MAISHANI MWAKO
Marko 4:18-19, “Hawa ndio wale waliopandwa penye miiba; hao ndio walisikiao Neno, na shughuli za dunia hii, udanganyifu wa utajiri, na tamaa za mambo mengine zikiingia hulisonga Neno, nalo halizai.” Enyi watu wa Mungu, tumesikia mahubiri mengi, tumesoma Maandiko mengi lakini je, Neno la Mungu limezaa matunda maishani mwenu? Ikiwa Neno la Mungu halizai matunda, hebu tuwe wakweli - tatizo haliko kwake, tatizo liko kwako, au kwa kulenga zaidi, tatizo liko ndani yako kwa sababu ushahidi kwamba Neno la Mungu…
KUJILINGANISHA HUKUIBIA KURIDHIKA
1 Timotheo 6:6-9, “Bali kumcha Mungu na kuridhika ni faida kubwa. Kwa maana hatukuja na kitu cho chote hapa duniani, wala hatuwezi kutoka na kitu. Lakini kama tuna chakula na mavazi, basi tutaridhika. Watu wanaotamani kuwa matajiri huanguka katika majaribu na mtego na katika tamaa nyingi mbaya na za kijinga, ambazo huwatokomeza wanadamu katika upotevu na maangamizi.” Watu wa Mungu, ingawa jaribu la kujilinganisha na jirani zako limekuwa mtego wa ibilisi, leo mtandao umepanua ulinganisho wetu hadi kiwango cha kimataifa.…
MATOKEO YA KUTAMANI
Luka 12:15, “Akawaambia, ‘Jihadharini na kutamani, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu alivyo navyo.’” Watu wa Mungu, tunaishi katika ulimwengu ambapo wengi huamini udanganyifu muovu wamba uzima kweli umo katika wingi wa mali zao. Kama ilivyokuwa, ndivyo ilivyo. Ndiyo maana Bwana wetu Yesu Kristo alionya dhidi ya dhambi ya kutamani – tamaa ya kimwili ya kitu ambacho ni cha mtu mwingine inayokuangusha kwenye njia tupu ya kutoridhika. Kinachotupeleka hapo ni mtego wa kujilinganisha – huchochea kutamani, hivyo…
LINDA KILE AMBACHO SHETANI HAWEZI KUGUSA
1 Yohana 2:15-17, “Msiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani - tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima - hakitokani na Baba bali hutokana na dunia. Na dunia inapita pamoja na tamaa zake; bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu hukaa milele.” Watu wa Mungu, fikirini kile kinachowatia wasiwasi au kuwashughulisha sana. Tukijifunga kupita kiasi kwa mambo ya dunia hii, tunalemewa nayo. Usijifunge sana kwa kitu ambacho…
HATARI YA KUSHIKAMANA KUSIKOFAA
1 Wakorintho 7:29-31, “Nikisema hivyo ndugu zangu, nina maana kwamba muda uliobaki ni mfupi. Tangu sasa waliooa waishi kama hawakuoa; 30 na wana oomboleza kama hawaoombolezi; wenye furaha kama hawana furaha; wanaonunua kama walivyonunua si mali yao; 31 na wanaoshughulika na vitu vya dunia hii, kama hawahusiki navyo. Kwa maana dunia hii kama tunavyoiona sasa inatoweka.” Tunamshukuru Mungu kwa wingi wa rehema zake ambazo tumezipata katika mwaka unaoisha, na tunaamini unatarajia kuona utimilifu wa kile ambacho Mungu ameweka moyoni mwako…