“Kile ambacho moyo wako umekishikilia kinaweza kukukamata kwa urahisi. Tunaposhikilia Neno la Mungu mioyoni mwetu, hugeuka kuwa ngome yetu.”

Katika mzunguko wa shughuli za kila siku, tunapataje wasaa wa kutunza maisha yetu ya kiroho? Pamoja na nguvu nyingi kinzani zinazopigania usikivu wetu, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kutumia muda bora kila siku katika Neno Hai la Mungu – chanzo kimoja cha ukweli na uthabiti tunachoweza kukitegemea kila wakati! Kama vile Mathayo 24:35 inavyosema, “Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” Unaposoma machapisho haya yenye mwongozo juu ya kujitoa kwa Mungu kutoka kwa Timu ya God’s Heart TV, tunaomba kwamba Mungu afungue moyo wako kwa hekima Yake na kukusaidia kuona maisha kwa udhahiri – kupitia macho Yake.

NJIA BORA YA KUSIMAMIA HAZINA

Mathayo 6:20-21, “Bali jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba. Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.” Enyi watu wa Mungu, kama wageni na wasafiri duniani, tunapotumia vitu vya ulimwengu huu, hatupaswi kujihusisha navyo. Wengi hufuatilia na kujiwekea hazina duniani - vitu wanavyotaka lakini hawavihitaji sana, vitu vinavyopungua thamani pale nondo na kutu vinapoharibu. Katika Luka 12:16-21, Yesu alitoa onyo kali kuhusu hatari za kujiwekea hazina bila kuwa tajiri kwa Mungu…

Soma Zaidi »

USIYASONGE MATUNDA YA NENO LA MUNGU MAISHANI MWAKO

Marko 4:18-19, “Hawa ndio wale waliopandwa penye miiba; hao ndio walisikiao Neno, na shughuli za dunia hii, udanganyifu wa utajiri, na tamaa za mambo mengine zikiingia hulisonga Neno, nalo halizai.” Enyi watu wa Mungu, tumesikia mahubiri mengi, tumesoma Maandiko mengi lakini je, Neno la Mungu limezaa matunda maishani mwenu? Ikiwa Neno la Mungu halizai matunda, hebu tuwe wakweli - tatizo haliko kwake, tatizo liko kwako, au kwa kulenga zaidi, tatizo liko ndani yako kwa sababu ushahidi kwamba Neno la Mungu…

Soma Zaidi »

KUJILINGANISHA HUKUIBIA KURIDHIKA

1 Timotheo 6:6-9, “Bali kumcha Mungu na kuridhika ni faida kubwa. Kwa maana hatukuja na kitu cho chote hapa duniani, wala hatuwezi kutoka na kitu. Lakini kama tuna chakula na mavazi, basi tutaridhika. Watu wanaotamani kuwa matajiri huanguka katika majaribu na mtego na katika tamaa nyingi mbaya na za kijinga, ambazo huwatokomeza wanadamu katika upotevu na maangamizi.” Watu wa Mungu, ingawa jaribu la kujilinganisha na jirani zako limekuwa mtego wa ibilisi, leo mtandao umepanua ulinganisho wetu hadi kiwango cha kimataifa.…

Soma Zaidi »

MATOKEO YA KUTAMANI

Luka 12:15, “Akawaambia, ‘Jihadharini na kutamani, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu alivyo navyo.’” Watu wa Mungu, tunaishi katika ulimwengu ambapo wengi huamini udanganyifu muovu wamba uzima kweli umo katika wingi wa mali zao. Kama ilivyokuwa, ndivyo ilivyo. Ndiyo maana Bwana wetu Yesu Kristo alionya dhidi ya dhambi ya kutamani – tamaa ya kimwili ya kitu ambacho ni cha mtu mwingine inayokuangusha kwenye njia tupu ya kutoridhika. Kinachotupeleka hapo ni mtego wa kujilinganisha – huchochea kutamani, hivyo…

Soma Zaidi »

LINDA KILE AMBACHO SHETANI HAWEZI KUGUSA

1 Yohana 2:15-17, “Msiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani - tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima - hakitokani na Baba bali hutokana na dunia. Na dunia inapita pamoja na tamaa zake; bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu hukaa milele.” Watu wa Mungu, fikirini kile kinachowatia wasiwasi au kuwashughulisha sana. Tukijifunga kupita kiasi kwa mambo ya dunia hii, tunalemewa nayo. Usijifunge sana kwa kitu ambacho…

Soma Zaidi »

HATARI YA KUSHIKAMANA KUSIKOFAA

1 Wakorintho 7:29-31, “Nikisema hivyo ndugu zangu, nina maana kwamba muda uliobaki ni mfupi. Tangu sasa waliooa waishi kama hawakuoa; 30 na wana oomboleza kama hawaoombolezi; wenye furaha kama hawana furaha; wanaonunua kama walivyonunua si mali yao; 31 na wanaoshughulika na vitu vya dunia hii, kama hawahusiki navyo. Kwa maana dunia hii kama tunavyoiona sasa inatoweka.” Tunamshukuru Mungu kwa wingi wa rehema zake ambazo tumezipata katika mwaka unaoisha, na tunaamini unatarajia kuona utimilifu wa kile ambacho Mungu ameweka moyoni mwako…

Soma Zaidi »