“Kama Wakristo, ni jukumu takatifu kuwajali wasiojiweza kati yetu.”

Mojawapo ya misheni ya msingi ya God’s Heart TV ni kushiriki upendo wa Mungu katika miradi ya hisani, tukijua kwamba ushahidi wa upendo wetu kwa Mungu ni kufurika kwa upendo huo kwa wengine.

Hizi hapa ni baadhi ya ripoti kutoka kwenye miradi ya hivi majuzi ya misaada ya kibinadamu ya God’s Heart TV, ambayo imefanyika katika mataifa kama vile Colombia, Honduras, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Meksiko, Kazakhstan na Uingereza. Unaweza pia kutazama video fupi za hali halisi ya baadhi ya miradi hii hapa.

TUKIO LA UTOAJI LILILOFANYA NA TELEVISHENI YA MOYO WA MUNGU (GOD’S HEART TV) SIKU YA  KRISMASI NCHINI  UINGEREZA!

Upendo ulizaliwa kwenye Krismasi! Kwa heshima ya msimu wa Krismasi, Timu ya TV ya Moyo wa Mungu (God’s Heart TV) ilinunua na kupanga mifuko 30 iliyosheheni vyakula na vitafunwa kwa ajili ya sherehe. Kila zawadi pia iliambatanishwa na kadi ya Krismasi iliyoandikwa kwa mkono yenye ujumbe wa kutia moyo na kisha kupelekwa kwenye shule kadhaa karibu na Manchester, Uingereza, ili kutolewa kwa familia zisizo na uwezo katika jumuiya ya eneo hilo. Tunamshukuru Mungu kwa nafasi ya kushiriki na kuonyesha upendo…

Soma Zaidi »

SAFARI YA TELEVISHENI YA MOYO WA MUNGU (GOD’S HEART TV) KUELEKEA INDIA KWA AJILI YA MSAADA WA KIBINADAMU!

Timu ya Televisheni ya Moyo wa Mungu (God's Heart TV) iliwasili hivi majuzi kutoka kwenye mradi wa kibinadamu katika taifa la India ambapo tulipata fursa ya kuunga mkono kazi ya Kanisa la Betheli la DGM katika eneo la Udupi katika Jimbo la Karnataka. Huduma hii hutoa msaada na ukarabati wa  masaa 24 siku zote 7 za juma kwa wagonjwa 85 wanaokabiliwa na changamoto kubwa za kiakili na kimwili na kwa upenda, wanalea watoto 13 katika kituo chao cha kulelea watoto…

Soma Zaidi »

MAFURIKO NCHINI PAKISTAN: ZIARA YA KIBINADAMU YA TELEVISHENI YA MOYO WA MUNGU (GOD’S HEART TV)!

Baada ya mfululizo wa mafuriko makubwa kulikumba taifa la Pakistani mnamo Agosti na Septemba 2025, Televisheni ya Moyo wa Mungu (God’s Heart TV) ilituma rasilimali za kifedha kwa wizara ya eneo la Lahore, Pakistani, ili kutoa chakula muhimu kwa familia 200 ambazo ziliathiriwa na mafuriko. Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka kwenye ziara hii ya msaada wa kibinadamu - kwa ajili ya utukufu wa Mungu! Tunamshukuru Yesu Kristo kwa nafasi ya kushiriki kivitendo upendo wa Mungu kwa wale wanaohitaji.…

Soma Zaidi »