Sera ya Faragha
Inatumika tangu : Jan 2022 Sasisho la Mwisho: Machi 2024
UKUSANYAJI WA TAARIFA BINAFSI: Timu ya God’s Heart TV hukusanya taarifa binafsi unazotoa. Tunakusanya data yako kuhusiana na fomu yoyote unayojaza kwenye tovuti (godsheart.tv) na kuitumia kwa ajili tu ya kutimiza malengo yetu ya kuendeleza Imani ya Kikristo.
TOVUTI NA COOKIES: Hatukusanyi taarifa binafsi zozote juu ya ziara zako za kuzuru kwenye Tovuti. Taarifa binafsi pekee tunazokusanya ni zile unazotupatia kupitia barua-pepe, simu, WhatsApp, au kwa kujibu mojawapo ya fomu zilizo kwenye Tovuti.
MAUDHUI YALIYOJUMUISHWA: Baadhi ya kurasa kwenye tovuti hii zinaweza kujumuisha maudhui yaliyojumuishwa (mfano. Video) kutoka tovuti nyingine. Haya hufanya kazi kwa njia ile ile kana kwamba mgeni ametembelea tovuti nyingine. Tovuti hizo zinaweza kukusanya data juu yako, kutumia cookies, kujumuisha ufuatiliaji wa ziada wa wadau wengine, pamoja na kufuatilia mwingiliano wako ikiwa una akaunti na umeingia kwenye tovuti hiyo.
UHIFADHI WA DATA YAKO: Tunahifadhi taarifa zako binafsi kwa muda unaohitajika tu kwa maudhumuni uliyotoa. Tunaheshimu maombi yote ya watumiaji ya kufuta data zao binafsi.
UHAMISHO WA DATA YAKO KWA WENGINE: Isipokuwa kwa data inayohitajika kushughulikia michango (tazama Taarifa za Kifedha hapa chini), data yako haitolewi kwa shirika lolote jingine, wala haitumiki kwa madhumuni ya kibiashara.
USALAMA WA DATA: Data huhifadhiwa kwa usalama, na wale wote wanaofanya kazi na timu ya God’s Heart TV hupewa maelekezo kwa umakini juu ya kuheshimu faragha ya taarifa wanazoziona.
TAARIFA ZA KIFEDHA: Unapotumia jukwaa hili kutoa mchango, tutakusanya jina lako, anwani ya barua-pepe, na ujumbe wowote uliouweka kwenye sehemu ya maoni. Hatuna namna ya kuzifikia taarifa zako za kifedha, ambazo husimamiwa kwa usalama na mfumo wa malipo au wakala wa kadi ya malipo. Tunawashirikisha Fundraise Up tu kwa madhumuni ya utoaji wa huduma.
MABADILIKO YA SERA HII YA FARAGHA: Endapo God’s Heart TV itabadilisha Sera yake ya Faragha, mabadiliko hayo yatachapishwa mahali hapa.
TAARIFA ZA ZIADA: Ikiwa una maswali yoyote zaidi kuhusu Sera yetu ya Faragha, tafadhali wasiliana nasi kupitia privacy@godsheart.tv
TAARIFA ZA KIBIASHARA: God’s Heart TV ni shirika lisilo la kifedha, lililosajiliwa nchini Uingereza. Nambari ya Kampuni ni 13961468 na Anwani ya Ofisi iliyosajiliwa ni 23 Trinity Square, Llandudno, LL30 2RH.