“Ibilisi anachukia ushuhuda kwa sababu ni silaha ya kuondosha udanganyifu wake.”

Nguvu za Mungu za kuponya, kukomboa, kurejesha na kuokoa hazijabadilika na umbali sio kizuizi kwa Roho Wake! Hapa unaweza kusoma baadhi ya shuhuda nzuri tunazopokea kila siku kwenye God’s Heart TV, ambazo tunaamini zitaimarisha imani yako.

Unaweza kutazama ushuhuda zaidi katika mfumo wa video hapa.

Ikiwa Mungu amegusa maisha yako kupitia huduma ya God’s Heart TV na una ushuhuda wa kushirikisha, tungependa kusikia kutoka kwako. Unaweza kushirikisha ushuhuda wako:

SIWEZI KUELEWA BADO ILIVYOFANYIKA!

“Nawasalimu katika jina la Yesu! Jina langu ni Asante kutoka Malawi, nataka kushuhudia wema wa Mungu na alichonifanyia. Kwa neema ya Mungu, Nilialikwa katika maombi ya ushirika mwaka wa 2025 karibu na 2026, ambapo tuliambiwa tuandike tunachotaka Mungu atufanyie mwaka ujao, 2026. Baadhi ya maombi yangu, niliandika kuwa nilitaka Mungu anisaidie katika kazi yangu na anipe ajira njema kuliko niliyo…

Soma Zaidi »

MUNGU AMEKUWA NAMI KATIKA HALI ZOTE!

“Neema na amani iwe nanyi nyote watu wa Mungu. Jina langu ni Sopheyclae kutoka Kenya. Niliigundua ibada ya maombi ya ushirika katika God’s Heart TV mwezi wa Oktoba 2024 wakati nilikuwa katika mapito. Familia yangu ilikuwa inapitia changamoto nyingi na hatukuwa na amani nyumbani. Tangu nijiunge na maombi haya,amani imerejea kati yangu na wazazi wangu na hata kwa ndugu zangu.Nataka…

Soma Zaidi »

MUNGU AMEBADILISHA MAISHA YANGU YA KIROHO!

“Watu wa Mungu niungeni katika kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake maishani mwangu. Jina langu ni Fred kutoka Ghana. Ushuhuda wangu ni huu: Nilianza kujiunga na maombi shirikishi ya Ndugu Chris katika God’s Heart TV mwaka wa 2024, naye Mungu akaanza kuyabadilisha Maisha yangu ya kiroho. Nilikuwa na wasiwasi na jakamoyo haswa kuhusu hali yangu ya umaskini na ugumu maishani, ambayo…

Soma Zaidi »

KUHITIMU KWA BINTI YANGU NI ISHARA YA NGUVU ZA MAOMBI HAYA!

"Jina langu ni Rhoda kutoka Kenya. Nataka kumpa Mungu utukufu kwa mambo mazuri aliyotenda maishani mwangu na katika familia yangu. Leo nasimama hapa kama shahidi wa nguvu za maombi na uzuri wa Mungu. Mwaka uliopita, nilituma ombi la maombi kwa God’s Heart TV na ninafuraha kuwatangazia kwamba Mungu ameyajibu maombi kwa njia kuu. Binti yangu alikuwa anasomea chuo kikuu cha…

Soma Zaidi »

HAYA NI MATENDO YA MUNGU NA YANAPENDEZA KWA MACHO!

“Nawasalimu nyote. Amani na neema kwenyu nyote. Jina langu ni Mary kutoka USA. Nataka kushuhudia wema wa Mungu. Mwaka uliopita nilikuwa na wasiwasi na woga mwingi. Katika serikali iliyoko USA saa hii, hatuna uhakika katika suala la kusafiri katika nchi nyingine. Hata walio vyuo vikuu wanalalamikia hilo licha ya kuwa na hati zinazofaa, kuingia nchini kunaweza kuwa na tatizo. Kama…

Soma Zaidi »

NAMPA MUNGU UTUKUFU KWA NEEMA YAKE MAISHANI MWANGU!

“Jina langu ni Judita kutoka Slovenia. Niliwasiliana na God’s Heart TV mara kadhaa kwa ajili ya maombi. Mambo yalikuwa mabaya na yalionekana kutobadilika. Lakini baada ya kujiunga na maombi ya ushirika nina shuhuda tele ninazotaka kuwaelezea! Nimepata kazi na ni ajira inayodumu. Mama yangu alikuwa na changamoto kali ya kiafya na kwa sasa amepona. Nilikuwa katika ajali lakini Mungu aliniokoa.…

Soma Zaidi »

UKOMBOZI KUTOKA KWA MAWAZO YA KUJITIA KITANZI NA UNYOGOVU!

“Nawasalimu nyote katika jina la Yesu Kristo. Jina langu ni Mwaka kutoka Zambia na ningetaka kushuhudia wema wa bwana wetu, Yesu Kristo. Mwezi Januari 2024 nilianza kujihisi mnyonge mwilini na sikuwa na hamu ya kula. Baadaye mwezi wa Mechi, nilikuwa na uzito moyoni mwangu, na nilikuwa na huzuni tele na sikuweza kutambua kilichonitatiza. Mwishowe dalili zilianza kuwa mbaya. Nilishindwa kulala…

Soma Zaidi »

NDUGU CHRIS ALIPOOMBA, NILIPONA PAPO HAPO!

“Jina langu ni Saimone kutoka New Zealand. Amani ya Mungu iwe nawe Ndugu Chris na nawatakia mwaka mpya wa baraka 2026 nyinyi wote katika God’s Heart TV. Nataka kutoa ushuhuda kuhusu kupona kwangu katika jicho langu la kulia papo hapo baada ya kuhudhuria ibada ya Maombi ya Ushirika kupitia zoom siku ya jumapili,tarehe 28 mwezi wa Desemba 2025( wakati wa…

Soma Zaidi »

NILIJIFUNGUA MTOTO MSICHANA MWENYE AFYA NJEMA!

“Jina langu ni Tshepang kutoka Afrika Kusini. Nataka nimuimbie sifa Bwana kwa mwongozo na ulinzi wake siku zote za ujauzito wangu hadi siku nilipojifungua. Kama si maombi niliyopokea kutoka God’s Heart TV, sidhani kama ningekuwa hapa na mtoto wangu. Mungu amenitendea na milele nitashukuru kwa zawadi ya ajabu niliyoipokea. Huu ndio ushuhuda wangu! Jumatatu, 22 Disemba 2025, nilikuwa niende kuona…

Soma Zaidi »

SIKU TATU BAADA YA YA MAOMBI YA 2026, HEDHI YANGU ILIANZA!

“Habari za asubuhi na mshinde leo. Jina langu ni Chiko kutoka Zambia. Tatizo nililokuwa nalo ni kukoma kwa hedhi kwa miaka minne. Tarehe 27 Disemba 2025, nilihudhuria maombi ya moja kwa moja na tukaomba pamoja kwa ajili ya mwaka wa 2026. Siku tatu baada ya maombi hayo, hedhi yangu ilianza! Nataka tu nimshukuru Yesu Kristo kwa ukombozi niliopokea. Asante, Brother…

Soma Zaidi »

SIFIKIRII TENA KUPITA KIASI AU KUENDEKEZA MAWAZO HASI!

Neema na amani iwe kwenu katika jina la Yesu. Jina langu ni Letisia kutoka Namibia. Nataka kushuhudia wema wa Mungu na yale aliyonitendea kupitia mtumishi wake, Ndugu Chris. Nilikuwa katika kifungo cha mfadhaiko kilichoanza mwaka 2023. Kila mwaka, mzunguko huo ulijirudia tu. Hali hii ilinifanya nifikirie kupita kiasi, jambo lililosababisha mapigo ya moyo, kuchanganyikiwa, na mawazo hasi. Iliniathiri sana nikiwa…

Soma Zaidi »