“Nawasalimu nyote katika jina la Yesu Kristo. Jina langu ni Mwaka kutoka Zambia na ningetaka kushuhudia wema wa bwana wetu, Yesu Kristo. Mwezi Januari 2024 nilianza kujihisi mnyonge mwilini na sikuwa na hamu ya kula. Baadaye mwezi wa Mechi, nilikuwa na uzito moyoni mwangu, na nilikuwa na huzuni tele na sikuweza kutambua kilichonitatiza. Mwishowe dalili zilianza kuwa mbaya. Nilishindwa kulala na nikapatwa na maradhi ya kukosa usingizi. Nilianza kuwa na fikira hasi na nilisikia sauti ikiniambia, ‘hautawezi kutoka katika taabu hii,’ na pia nilikuwa na fikira za kujitoa kitanzi. Nilikuwa na wasiwasi iliyonisababisha hofu kila mara. Nilikuwa naona vivuli na vitu ya kustaajabisha katika ndoto zangu vilivyofanana na Wanyama hawa: mbwa, simba na nyoka. Nilikuwa na maumivu ya mgongo na hewa ilitoka nisiyoweza kuidhibiti. Nilikuwa na jinamizi ambazo niliwaona watu wakizuia njia yangu na wakiufunga mdomo wako.“Nilipokuwa katika mtandao niliiona tovuti ya God’s Heart TV. Niliposoma shuhuda nilielekea katika Whatsapp na nikajiunga nao na nikatuma ombi la maombi. Mwezi wa Julai 3, Nilialikwa katika ibada ya maombi ya ushirika kupitia Zoom. Niliomba nao siku hiyo. Nikajiunga tena nao Oktoba 4. Katika maombi yale, sikuhisi kitu chochote lakini baada ya siku moja ama mbili nilihisi Mungu akinigusa. Nilianza kudhihirisha mapepo yale! Miguu na mikono yangu ilikuwa ikitetemeka kwa siku mbili. Tuliendelea kuomba na hatimaye nilitapika kitu cha kahawia. Kwa sasa niko huru! Ninakula, ninalala vizuri na sina maumivu yale wala jinamizi. Watu wa Mungu, nastaajabu wema wa Mungu maishani mwangu. Asante Yesu. Kwa ndugu Chris nanena baraka na hekima kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwa timu yote ya God’s Heart TV – muwe salama nyote. Mungu mwema aendelee kuwajaza na hekima na neema tele. Asante sana Mungu.”