“Neema na amani iwe nanyi nyote watu wa Mungu. Jina langu ni Sopheyclae kutoka Kenya. Niliigundua ibada ya maombi ya ushirika katika God’s Heart TV mwezi wa Oktoba 2024 wakati nilikuwa katika mapito. Familia yangu ilikuwa inapitia changamoto nyingi na hatukuwa na amani nyumbani. Tangu nijiunge na maombi haya,amani imerejea kati yangu na wazazi wangu na hata kwa ndugu zangu.Nataka pia kushuhudia kwamba kaka yangu alifanya mtihani wake wa kufunga mwaka mwezi wa Oktoba. Kwa neema ya Mungu, amepita mtihani wake na amejiunga na kidato kinachofuata. Pia, najihisi mbarikiwa tangu kujiunga na maombi kwa kuwa nilitamani kuanza biashara ya mtandao. Mungu aliyajibu maombi yangu mwezi wa Januari na sijawahi kosa wateja. Nina amani maishani mwangu. Mungu amekuwa nami katika hali zote! Mawaidha yangu kwa watu wa Mungu ni kutoka kitabu cha Isaya 45, ambapo Mungu alimteua Sairasi na kumwahidi kuwa atamfungulia milango na miji, atatengeneza njia kwa kuisawazisha milima. Mungu ataivunja milango ya shaba na kuzing’oa chuma, ili kuwapa hazina zilizofichwa katika siri na giza. Mbarikiwe!”