“Amani na neema kwa familia ya God’s Heart TV. Jina langu ni Lydia kutoka Zambia. Sikujua Mungu atanibariki hivi kupitia Ndugu Chris. Amenifanyia mambo ya ajabu na najua hajamalizana nami. Nilijiunga na maombi ya ushirika ya God’s Heart TV mwaka wa 2023 ila sikuona kufanikiwa maishani mwangu na kwa hilo nikafa moyo nikawacha kuzingatia maombi ya God’s Heart tv. Nilichanganyikiwa na kuzidiwa. Nilidhani kwamba majibu yangu yatakuja kwa kasi bila kutambua kuwa Mungu alikuwa ananiandaa. Baadaye,nilianza kutuma ombi la maombi kwa God’s Heart TV tena 2025 licha ya kuwa mara nyingi nilikubwa na changamoto za kimtandao. Mwishowe, kwa neema ya Mungu niliweza kujiunga kupitia Youtube na nimeufanya mtindo wangu kuomba na maombi ya moja kwa moja kila asubuhi na jioni. Baadhi ya shuhuda zangu ni hizi:

1.Binti yangu alipata udhamini katika chuo kwa miaka miwili na pia amepata nafasi ya kuwa baadhi ya wanafunzi wale ambao watakaofanya mitihani yao ya mwisho wa mwaka huu.

2.Mwana wangu amepata ufadhili wa serikali ili aendeleze masomo yake ya kiwango cha juu alipowasilisha licha ya kuwa kulikuwa na mchakato mgumu lakini Mungu alitufanyia muujiza hatimaye.

3.Katika mwezi wa Agosti, nilimtembelea dada yangu mdogo na usiku mmoja maisha yangu yalififia na nikaondoka mapema. Lakini kijana mmoja mtanashati aliniambia nirudi akiniambia wakati wangu haukuwa umetimia. Mahali pale palikuwa panapendeza lakini kwa kuwa wakati wangu haukuwa umetimia ilibidi nirudi.

4.Katika mwezi wa Oktoba, kaka yangu alipitia changamoto na alikubwa na mafikira ya kujiua. Hata kama si wa Imani yetu, nilimtumia tovuti la God’s Heart TV na akaomba na kwa sasa ametulia.

5.Dada yangu alikuwa mjamzito na alikuwa na viwango vidogo vya damu ambavyo vilifanya apate rufaa katika hospitali ya juu. Katika harakati ile alipoteza Imani na akatamani kufa. Nilipeleka jambo hili kwa Mungu kwa niaba yake na kwa miujiza alijifungua kwa muda mchache bila changamoto yoyote.

6.Dada yangu, mzaliwa wa mwisho, alinusurika katika ajali ya barabara.

“Kile ambacho kimesalia ni kumshukuru Yesu Kristo.” Najua kazi yake maishani mwangu haijamalizika na kwa neema ya Mungu nitarejaea na shuhuda nyingine kwa utukufu wa Mungu. Asante sana Ndugu Chris na timu ya God’s Heart TV.”