“Neema na amani iwe nanyi nyote katika God’s Heart TV. Nataka kumshukuru Mungu kwa Maisha ya Ndugu Chris na kwa kujisalimisha ili atumike na Mungu. Jina langu ni Elias kutoka Mozambique. Kwa wakati huu nataka kutoa ushuhuda! Sijui ningekuwa wapi ikiwa Mungu hangejidhihirisha katika Maisha yangu. Kwa miaka minne, nilikuwa sina ajira. Niliwasilisha hati zangu katika kampuni nyingi lakini hakuna lililiofanyika, sikupata jibu la kuridhisha. Kwa sababu ya kutoajiriwa, nilipitia mapito mengi -njaa, kudharauliwa, kukataliwa. Nilipoteza vitu vingi; hata mpenzi wangu aliniacha na familia yangu, hakuna mtu alinipa msaada. Ilifika wakati nikapata unyogovu; sikujali mwonekano wangu wala sikuwa na matumaini. Nilidhani Mungu ameniacha. Siku moja niliona chapisho katika Facebook ya God’s Heart TV, na nikawasilisha ombi langu la maombi la kujiunga na Maombi ya Ushirika. Ilikuwa siku ya Desemba 27, 2025, ambapo Ndugu Chris alituhimiza tuandike mahitaji yetu kwa maombi. Niliandika ombi langu la kutaka kupata ajira ya kudumu. Imekuwa mwezi mmoja kwa sasa na nimepata ofa za ajira katika kampuni tatu! Siwezi kuamini. Nina hisia nyingi moyoni mwangu – Mungu alisikia kilio changu na kuyapanguza machozi yangu. Amenipa pumziko kuu licha ya fedheha niliyopitia. Najua kuwa ni Yesu Kristo amenitendea muujiza huu. Nina furaha na sina lolote ila kumshukuru Mungu na Ndugu Chris. Nashukuru sana kutoka kwa mtima wangu. Asante!”