“Neema na amani kwenu nyote. Jina langu ni Saraphina kutoka Ghana. Nataka kushuhudia wema wa Mungu katika familia yangu. Niliijua huduma hii kupitia mume wangu baada ya kupoteza ujauzito wangu Novemba 2024 na kwa hilo,nilikuwa na huzuni. Tangu siku hiyo, nimekuwa nikihudhuria ibada ya maombi ya ushirika kila mwezi kupitia Zoom. Januari 2025, nilijiunga na maombi ya ushirika tena na nilikuwa na maombi haya mawili:
1.Nipate ujauzito tena.
2.Nipandishwe cheo kutoka kuwa msimamizi wa polisi II hadi kuwa msimamizi mkuu nitakapowasilisha shahada zangu.

“Februari 2025, tovuti letu lilifunguliwa ili wale wenye shahada waziwasilishe ili wapate kupandishwa cheo, niliwasilisha Pamoja na wenzangu. Mnamo Mei 2025, kwa utukufu wa Mungu nilipandishwa cheo. Kupandishwa cheo huku huchukua hata mwaka mmoja ama zaidi lakini kwangu, Mungu alinirahisishia njia yangu. Ushuhuda wangu wa pili ni huu: nilipata ujauzito tena lakini nikaanza kutokwa damu, hili lilikuwa jambo hatari kwa ujauzito wangu. Lakini, Mungu alimlinda mtoto wangu hadi Januari 3, 2026 ambapo nilijifungua binti mrembo kwa utukufu wa Mungu. Tulimpa jina Wemanga kumaanisha ‘wakati wa Mungu’. Nataka kuwatia moyo nyote kwa kuwasihi mumwamini Mungu na kuiweka Imani yenu hai kwa kuwa, katika wakati wa Mungu kila jambo litafanikishwa!”