“Salamu kwa jina la Yesu Kristo, jina langu naitwa Natalia nakuandikia kutoka Sweden, niliwasiliana na God’s Heart TV Mei 2024, nilipohitaji maombi kwa sababu nilikuwa mjamzito na nilikuwa nikitokwa na damu nyingi kwa sababu ya maradhi ya hematoma kwenye uterasi. Mimba yangu ilikuwa hatarini kuharibika.

Ndugu Chris, aliniombea na kunitia moyo niendelee kusali na kulifanya Neno la Mungu kuwa msingi wa maisha yangu. Muda mfupi baada ya maombi, nilienda kupima ultrasound, na walisema hapakuwa na dalili zozote za hematoma. Pia niliacha kutokwa na damu wiki chache baada ya maombi niliyopokea kutoka kwa Ndugu Chris.

Leo, nataka kumshukuru Bwana kwa wema wake na neema ambayo imeniweka hadi wakati huu. Mtoto huyo wa kike ambaye hapo awali alikuwa katika hatari ya kufa sasa ana umri wa miezi minne. Tulimwita Elinor kama ukumbusho kwamba Mungu ni Nuru yetu. Ninamshukuru sana Yesu Kristo kwa yale aliyonifanyia. Binti yetu mdogo alizaliwa mnamo Novemba, 2025, bila matatizo yoyote, licha ya matatizo niliyokuwa nayo wakati wa ujauzito. Asante sana mtu wa Mungu kwa muda wako na upendo wako kwa wana wa Mungu.”