“Neema na amani kwenyu nyote watu wa Mungu. Jina langu ni Vanessa kutoka Uganda. Nataka kumshukuru Mungu kwa kile alichofanya katika maisha ya wapendwa wangu. Kwa mwaka mmmoja na nusu, alisubiri kupata mkataba wa ajira – huu ulikuwa muda wa miezi kumi na minane uliojawa na hofu, maombi na kutokuwa na hakika na kuna wakati hakuna kitu kilichoonekana kufanyika. Wakati mwingi, kusubiri kule kulitupa wasiwasi lakini Mungu alikuwa akitenegeneza njia. Katika yote Mungu alimpa nguvu, subira na imani. Hata milango ilipoonekana kufungwa na matumaini kupotea, Mungu alikuwa mwaminifu. Katika wakati wa Mungu, mkataba ule ulifaulu! Muda ulioonekana kuwa wa Subira uligeuka na kuwa ushuhuda wa uvumilivu na wakati wa Mungu. Muda huu umetukumbusha kuwa Mungu hawezi sahau ahadi zake na kumsubiri si kupoteza muda tunapomwamini. Kwa yeyote, anaye subiri natumai umepata matumaini kwa Mungu – kwamba anatengeneza njia hata usipoona. Tunampa Mungu utukufu, heshima na shukrani kwa muujiza huu. Amina!