Tunafurahi kukutaarifu kwamba Ndugu Chris na Timu ya TV ya Moyo wa Mungu wamerejea hivi punde kutoka kisiwa cha Cuba ambako tulipata fursa ya kuwahudumia maelfu ya vijana waliosafiri kutoka kote nchini kushiriki katika hafla ya kitaifa ya vijana.

Mioyo na maisha ya wengi iliguswa na Roho Mtakatifu pale Neno la Mungu lilipotangazwa, nguvu za Mungu zilidhihirishwa na utukufu wa Mungu ukafunuliwa! Kongamano la vijana, lililochukua siku tatu, lilijumuisha shuhuda za kutoka moyoni, jumbe za kujenga imani, pindi zenye nguvu za maombi, kipindi cha maswali na majibu na ibada iliyoongozwa na Roho Mtakatifu. Televisheni ya Moyo wa Mungu (God’s Heart TV) pia ilifanya tukio la kutoa misaada ili kuzifikia familia 100 zenye maisha duni katika eneo jirani.

Huu ni wakati muhimu kwa huduma kwani ni mara ya kwanza kabisa kwa Mungu kumwachilia Ndugu Chris kusafiri kwa ajili ya huduma ya umma tangu kuzinduliwa kwa TV ya Moyo wa Mungu mnamo Januari 2022.

Asanteni nyote kwa upendo wenu unaoendelea, maombi na msaada! Ni pendeleo lililoje kushiriki katika miradi ya Mungu na kueneza Habari Njema ya Yesu Kristo katika pembe nne za dunia!