Timu ya Televisheni ya Moyo wa Mungu (God’s Heart TV) iliwasili hivi majuzi kutoka kwenye mradi wa kibinadamu katika taifa la India ambapo tulipata fursa ya kuunga mkono kazi ya Kanisa la Betheli la DGM katika eneo la Udupi katika Jimbo la Karnataka. Huduma hii hutoa msaada na ukarabati wa  masaa 24 siku zote 7 za juma kwa wagonjwa 85 wanaokabiliwa na changamoto kubwa za kiakili na kimwili na kwa upenda, wanalea watoto 13 katika kituo chao cha kulelea watoto yatima, na kuwahudumia ili wastawi kielimu, kihisia, kimwili na kiroho.

Kwa neema ya Mungu, na kwa ukarimu wa wabia wa TV ya Moyo wa Mungu (God’s Heart TV Partners), tulitoa mchango wa fedha taslimu, magodoro tisini ya ubora wa juu, mito na mashuka pamoja na vyakula ambavyo vitalisha wagonjwa na watoto kwa mwezi mzima. Mbali na bidhaa hizi muhimu, watoto walibarikiwa kwa kupewa vifaa vya michezo na vinyago kusaidia burudani ya kiafya na kucheza kwa uchangamfu. Timu yetu pia ilitoa vifurushi vya bidhaa za kujikimu kwa wafanyikazi 35 waliojitolea wanaohudumia wagonjwa hawa walio hatarini kwa bidii isiyoyumba na roho ya ubora. Kila kifurushi kilijumuisha mboga, mfuko wa mchele, na zawadi ya pesa taslimu.

Upendo hutazama pande zote ili kuona wale walio na uhitaji – hivyo mwombe Mungu akupe macho yake ili uwapate wale wanaokuhitaji zaidi. Hao hawana baba ili wewe uwe baba yao; wako katika uhitaji ili wewe uwe mfadhili wao.  Tunakualika uendelee kumuombea Mchungaji Sunil na timu yake karimu wanapopanua upendo, huruma, na kujali kwa vitendo kwa baadhi ya waliopuuzwa na wanaohitaji sana katika jamii.