“Nawasalimu nyote. Amani na neema kwenyu nyote. Jina langu ni Mary kutoka USA. Nataka kushuhudia wema wa Mungu. Mwaka uliopita nilikuwa na wasiwasi na woga mwingi. Katika serikali iliyoko USA saa hii, hatuna uhakika katika suala la kusafiri katika nchi nyingine. Hata walio vyuo vikuu wanalalamikia hilo licha ya kuwa na hati zinazofaa, kuingia nchini kunaweza kuwa na tatizo. Kama mtu aliye na visa ya mwanafunzi kwa mwaka mmoja ili nimalize shahada ya uzamifu katika eneo la Civil Engineering, jambo hilo lilinitia woga – hasaa kwa kuwa mume wangu wakati ule wa 2024 alikuwa amepanga kusafiri katika nchi yangu ili awaone wazazi wangu na tupate kuanza maandalizi ya harusi yangu. Tuliomba kila wakati, tukiamini kuwa utukufu wa Mungu utaenda mbele yetu na kwamba nitaweza kurudi USA bila shida ili nipate kumaliza masomo yangu na niwe karibu na mume wangu, ambaye ni mwananchi wa Amerika. Tulituma ombi la maombi kwa God’s Heart TV. Kwa neema ya Mungu, tulizungumza na Ndugu Chris na alichukua muda kututia moyo kama wanaharusi wapya na akatukumbusha tuishi kwa njia inayompendeza Mungu na pia tutii neno lake.
“Pia kwa kweli, nimeona neema ya Mungu. Tulisafiri Zambia vyema. Familia zetu ziliungana kwa upendo na amani. Sherehe za harusi zilipendeza na Mungu alitupa kila tulichohitaji katika harusi. Ushuhuda mwingine ni kuwa mimi na mume wangu tulipata nyumba nyingine. Kwa utukufu wa Mungu tumenunua samani za gharama ya $5,000 kwa $400 pekee. Wanandoa kutoka mji wa New Jersey walikuwa wakiondoka kwenda nchi nyingine na walituuzia vitu vyao vipya kwa pesa kidogo. Pia, baada ya harusi na kurudi U.S. Nilikamilisha mafunzo ya kazini ya miezi mitatu katika kampuni iliyoko NYC na nikapewa nafasi ya kazi nitakapomaliza uzamifu wangu mwezi wa Juni 2026. Bali na hayo, niliwasilisha green card mwezi wa Agosti na nikakubaliwa mwezi wa Novemba – kwa kipindi cha miezi mitatu! Mchakato unaochukua miaka miwili ama moja ulifanyika katika chini ya miezi mitatu. Haya ni matendo ya Mungu, na kwa kweli yanapendeza machoni. Muda huu umenivuta kwa Mungu. Katika wakati ule wa wasiwasi, niliomba, nilisoma Biblia na nikamwamini Mungu kwa ukamili. Pia nimeuona uaminifu wa Mungu. Utukufu wote uwe wa Mungu!”