“Jina langu ni Jean-Luc kutoka Ufaransa. Namshukuru Yesu kwa kuosha dhambi zangu katika kongamano la ‘Let Hearts Arise’ na God’s Heart TV kule Birmingham, Uingereza mwaka uliopita. Ndugu Chris aliniombea na kutangaza ‘Niko huru’ na kwa hakika niko huru leo kutoka kwenye minyororo ya uasherati na ponografia. Nashukuru timu yote ya God’s Heart TV kwa maombi, Faraja na msaada wenu hasaa katika kutusaidia kukongamana hapa, mbali na nyumbani. Maumivu yangu ya mgongo, kizunguzungu na kutokwa damu katika fizi kumetoweka. Damu yangu iko imara. Asante, Yesu! Sikuwa na ajira kwa miaka mingi lakini mpango wa Mungu ni kamili. Nina chakula cha kutosha na nina mahali pa kulala. Ninaamini kuwa huu ni wakati wa mabadiliko ambapo Mungu ananuia kunifanya kuelewa upuuzi wa mambo ya kidunia, ili kuitakasa roho yangu na kuanzisha uhusiano Naye katika moyo wangu – sehemu ya mawasiliano baina yetu na Roho mtakatifu. Muujiza wangu wa kazi utakuja baadaye; namwamini Yesu! Namshukuru Mungu kwa zawadi kuu ya mwaliko kupitia Zoom katika mikutano ya God’s Heart TV. Sisi sote ni familia moja kubwa. Sina upweke tena!”