“Amani na neema kwenyu nyote katika jina la Yesu na timu ya God’s Heart TV. Majina yetu ni Mercy and Messiah, na sisi ni mapacha kutoka Botswana. Tunataka kushuhudia jinsi Mungu alivyoyajibu maombi yetu kuhusu cheti cha mitihani midogo ya 2025 baada ya kujiunga na maombi ya ushirikishi na Ndugu Chris. Mwaka uliopita mnamo Oktoba 2025, tulifanya mitihani ya mwisho na tungetaka kushuhudia matokeo mema yaliyozidi matarajio yetu. Tulikuwa na changamoto katika Hisabati na tulipokuwa tukifanya mtihani wa pili tuliwacha maswali machache tupu. Lakini kwa neema ya Mungu, ametutendea mema. Kila siku tuliombea mtihani huo. Tulikuwa tunangojea matokeo machache kwa kuwa mtihani huo ulikuwa mgumu. Kinyume na matarajio yetu, matokeo yalipowasili tulikuwa tumepita sana. Tunashkurani sana kwa mafanikio haya!”