“Jina langu ni Asisipho kutoka South Africa. Nataka kushuhudia wema wa Mungu maishani mwangu. Mwaka uliopita, nilikuwa nafanya mtihani wa matric kwa mara nyingine(kidato cha 12, South Africa) kwa kuwa nilikuwa natumai kusoma sheria katika chuo kikuu. Singeweza kuifanya zamani kwa kuwa matokeo yangu yalikuwa machache. Katika mwaka wa 2025, nilialikwa kuomba na ndugu Chris kabla ya mwaka kuanza. Nilikuwa naomba nipate nafasi ya kusomea shahada ya sheria. Nilikuwa nimekataliwa na vyuo vikuu vingi na nilikata tamaa na kudhani matumaini yote yangu yamekwisha hadi nilipopata barua pepe katika simu yangu ya mojawapo ya vyuo vikuu vilivyonikataa kwa sababu sikufanikiwa kuwa na kiwango kilichotakikana. Nilifungua hati ile katika kompyuta yangu na iliashiria kuwa nilikuwa nimekubalika katika shahada ambayo hapo awali nilikataliwa kwa kuwa sikuwa na matokeo yaliyotakikana, shahada ambayo ilikuwa chaguo langu la kwanza. Sikuamini macho yangu kwa kuwa nilidhani ndoto yangu ya kuwa wakili haiwezekani lakini Mungu alinikumbuka na akanipa nafasi nyingine. Namshukuru Mungu kwa upendo wake usio na kifani na neema yake maishani mwangu. Pia, nilipata msaada wa kifedha na nikajiandikisha. Nilifanikiwa kwa kila kitu na nilijua ni Mungu kwa kuwa hakuna aliye na neema kama yeye. Natumai ushuhuda huu utampa mtu imani kwa Mungu. Amina.”