“Salamu katika jina la Yesu Kristo. Jina langu ni Greyford kutoka Zambia. Ushuhuda wangu ni kwamba wakati wa likizo za Pasaka, nilikuwa katika mkoa kwa Kaskazini Magharibi kwa ajili ya kazi. Aprili 4, 2026, ilipopita saa sita usiku kidogo, niliamshwa na mlio wa bunduki na kugoongwa kwa milango. Mifumo ya kufunga milango ilikuwa imepigwa risasi pia; watu walivurutwa nje na wakaamuriwa walale chini. Hii ilifanyika haraka sana kiasi ya kwamba wakati bado nilikuwa natafuta nguvu, walikuwa washafika kwenye mlango wangu, wakipiga risasi na wakinilazimisha nifungue mlango. Watoto wa Mungu, nilikuwa nimefunikwa na kuchanganyikiwa. Halafu nikatambua simu yangu ilikuwa inacheza maombi ya God’s Heart TV ya 24/7 kama ilivyokuwa desturi yangu ya kawaida usiku kucha, na nikaegemea maombi kama tumaini langu la mwisho. Hata kama akili yangu ilikuwa umefunikwa na uoga, wasiwasi na nilikuwa na kiwewe wakati nilikuwa najaribu kuweka akili sawa na maombi ya moja kwa moja, niliskia Brother Chris akisema, ‘Wacha kutazamia shida zako; weka mtazamo wako kwa Mungu.’ Ndugu, imani iliwaka ndani yangu kuanzia hapo. Waliita binti mmoja, mmoja wa wafanyakazi hapo, wakamuamuru awape ufunguo wa chumba changu. Akajibu, “Bwana, siwezi pata ufunguo huo.’ Badala ya kuipiga mfumo wa kufunga mlango risasi, waligeuza mawazo yao na wakarudi kwa wale ambao walikuwa nje tayari. Hivo ndivyo Yesu aliniokoa. Asubuhi, watu walikusanyika kujua hizo risasi zote zilikuwa kwa sababu gani na ndipo nilipojua ya kwanza timu spesheli ya ulinzi wa serikali ilikuwa imekuja kushika majambazi.
Ushauri wangu, ndugu na dada, ni maombi ya saa 24/7 hayafanyi kazi kwa muda tu; ni mapya kana kwamba yametoka kwenye benki la Roho Mtakatifu. Asante sana kwa Ndugu Chris na timu ya God’s Heart TV kwa kuruhusu mtumike kama vyomba vya kuaminiwa kwa mikono ya Yesu Kristo.”