Miongozo ya Ushuhuda
Hatua ya Kwanza – UTANGULIZI
- Tafadhali jitambulishe ukijumuisha jina lako la kwanza na nchi unayoishi
Hatua ya Pili – KABLA
- Ni changamoto gani ulizokuwa ukikabiliana nazo? Hii iliathirije maisha yako ya kila siku? Ulichukua hatua gani kutafuta suluhisho? Uligunduaje TV ya Moyo wa Mungu/ Ndugu Chris?
Hatua ya Tatu – MAOMBI:
- Ulipokeaje uponyaji/muujiza/ukombozi/mafanikio yako? Kitu gani haswa ulijisikia wakati huo (ikiwa kipo)?
Hatua ya Nne – BAADA:
- Ni mabadiliko gani katika maisha yako baada ya maombezi hayo? Maisha yako ya kiroho yamekuwaje tangu wakati huo?
Hatua ya Tano – USHAURI
- Ushauri au himizo lako ni nini kwa wengine wanaosikia ushuhuda wako?
UWASILISHAJI WA VIDEO:
Ikiwa utarekodi video ya kututumia, tunapendekeza utumie simu janja kurekodi ushuhuda wako. Kwa weredi zaidi, video yako ya awali ya ushuhuda inapaswa kuwa ya dakika moja hadi mbili. Tafadhali hakikisha:
- Mandhari yako ya nyuma ni nadhifu na yenye mwanga unaofaa.
- Mavazi yako ni ya heshima.
- Unaacha nafasi ya kutosha juu ya kichwa chako unapopiga picha.
- Ripoti/vifaa vyovyote vya kimatibabu unavyokusudia kuvionyesha katika ushuhuda vipo karibu nawe.
- Maneno yako ni fasaha na mafupi.
Tunatarajia kupokea ushuhuda wako mzuri – kwa utukufu wa Mungu!